FT: Azam FC 0-1 Yanga
Mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Azam Complex umekamilika kwa wenyeji Azam FC kuyeyusha jumla pointi tatu na kufungwa bao moja baada ya dakika 90 kukamilika.
Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Deus Kaseke dakika ya 48.
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 28 na kuwa nafasi ya kwanza jumlajumla.
Zimeongezwa dk 4
Dakika 90 zimekamilika
Dakika ya 87, Mnata anaanzisha mashambulizi
Dakika ya 78 Lamine Moro anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 62 Azam wanapeleka mashambulizi kwa Mnata
Dakika ya 58 Sure Boy anafanyiwa faulo na MukokoDakika ya 57 Kisinda anakosa ndani ya 18
Dakika ya 55 Lamine Moro anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 50 Sure Boy anapoteza mpira, Nchimbi anafanya jaribio linaokolewa na Kissu
Dakika ya 48 Kaseke Goooool
Dakika ya 47 Yanga wanaanzisha mashambulizi kwenda kwa kissu
Dakika ya 48 Kaseke Goooool
Dakika ya 47 Yanga wanaanzisha mashambulizi kwenda kwa kissu
KIPINDI cha pili kimeanza
UWANJA wa Azam Complex
Novemba 25
Ligi Kuu Bara
Azam FC 0-0 Yanga
Mapumziko
Zinaongezwa dakika 3
Dakika 43 Kissu anafanya save
Dakika ya 37 Yacouba anafanya jaribio linakwenda nje ya lango
Dakika ya 34 Djod anaonyeshwa kadi ya njano.
Dakika ya 27 Mnata anaokoa hatari
Dakika ya 26 Yassin anacheza faulo
Dakika ya 24 Prince Dube anafanyiwa mabadiliko ya lazima anaingia Djod
Dakika ya 23 Yacouba anaotea
Dakika ya 19 Lamine anaokoa hatari
Dakika ya 16 Dube anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 10 Azam wanapeleka mashambulizi kwa Mnata
Dakika ya 9 Nondo anaanua majalo
Dakika ya 8 Mudhathir anapaisha
Dakika ya 7 Dube anachezewa faulo
Dakika ya 6 Kissu anaokoa hatari
Dakika ya 5 Nchimbi anasababisha kona haizai matunda
Dakika ya 4 Mustapha Yassin anafanya jaribio
Walijiandaa kumkaba sarpong, Kaseke hajachuja nyie lambalamba!
ReplyDeleteSaleh Simba Jembe,mbona humalizi mechi?
ReplyDeleteMwandishi andika kilichopo. Yanga iko kileleni kwa sasa na si jumlajumla. Ligi bado sana
ReplyDeleteCedric Kaze akipata watu sahihi kama namba 8, 9 na 10 hii Yanga ya msimu huu ni hatari!
ReplyDeleteYule msemaji wa upande wa pili yuko?
ReplyDeleteAzam Ni ramba ramba kweli inaonyesha wachezaji hawachezi kwa Hari kabisa nadhani wachezaji wa Azam hawaitambui Azam Ni moja ya team yao iliowekeza na kuwalipa vizuri na kwa wakati na inataka ubingwa na naona benchi la ufundi la Azam hawakutambua kwamba sure boy anawahujumu huyo ndio alitakiwa awe wa Kwanza kutoka mudadhiri wangemuacha Kwanza halafu ilibidi alivyoumia dube iddi nado angeingizwa mapema sio kumuingiza yule mghana na tangu team ya Azam ianze kupoteza wachezaji hawana Hali kabisa ya upambanaji sijui Azam hawana daktari wa sciocology bado hawajakutana na Simba wajipange Mimi binafsi Azam nimeitoa kwa race za ubingwa nafasi kubwa kwa Simba na yanga kuchukua japo bado mapema
ReplyDeleteMaoni murua. Simba na Yanga waendelee kupambana nyuma yao yuko Mkwasa na Ruvu Shooting yake - gari limewaka huko. Kaze alikiri ndiye aliyetoa mapendekezo ya wachezaji waliosajiliwa na GSM. Kama bado hawaoneshi uwezo sahihi Yanga waliotamba wanao basi Kaze aliwaingiza chaka
DeleteMwamedi fc....tunawakumbusha tu.... point 5 zimeshawahusu.....so mwambie manara aka ukoko fc ajiandae kutushangilia tukinyanyua kwapa
ReplyDeleteKule msemaji mwenye mdomo kama mfuniko wa choo tunasubiri aropoke tena
ReplyDelete