November 22, 2020


 DILI la kujiunga na TP Mazembe ya DR Congo, la kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ limenoga zaidi huko Yanga, ambapo taarifa zimeeleza kuwa tayari viongozi wa klabu hiyo wameshawasilisha dau na kumnasa kwenye dirisha la usajili lijalo.

Mazembe wamezidi kuvutiwa na uwezo wa Fei Toto kiasi kwamba sasa wanasuburia tamko la Yanga tu ili waweze kumwaga pesa.


Chanzo kimeeleza kuwa hatimaye sasa Mazembe wameamua kuleta ofa maalumu kwa uongozi wa Yanga kuhusu kumsajili Fei.


“Ama kweli kila lenye mwanzo huwa halikosi mwisho, kwani pamoja na kuwepo na tetesi nyingi kiasi cha baadhi ya watu kubeza juu ya dili hilo, nikueleze tu kwamba mechi ya Stars imeongeza chachu ya TP Mazembe kumtaka Fei Toto.


“Kwani kilichobaki sasa ni kwetu viongozi kukubaliana juu ya ofa yao ili nasi tuweze kufaidi matunda ya kuuzwa kwake, TP Mazembe wametoa dau la Sh milioni 200 ili wavunje mkataba wake, ila sisi tunadhani wanatakiwa kuongeza hadi ifike Sh milioni 300 na kitu hivi ili tuwapatie jembe letu,” kilisema chanzo hicho.


Feti Toto alionyesha uwezo wa juu kiasi cha kuwavutia wengi katika mchezo wa Novemba 17 dhidi ya Tunisia, ambapo alifunga bapo la kusawazisha la Stars mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.


Chanzo:Spoti Xtra

7 COMMENTS:

  1. Hzo tetes zako subir uone majbu yake ndo ujue soka la bongo sio la kutoa taarifa za hovyoo

    ReplyDelete
  2. Hakika anastahili kutumikia club kubwa km tp mazembe maana anauwezo binafsi

    ReplyDelete
  3. Fei Toto alisajiliw kwa pea kidogo tu, ameiingizia yanga pesa nyingi tu.sasa kung'ang'ana na mil 300 ni kutaka kumbania mtoto wa watu ridhki.

    ReplyDelete
  4. Hiyo mnayotaka ni bei chee kutokana na kiwango chake . Mnyama yupo tayari kuongeza kuliko hizo mlizoomba Jee mutampa?

    ReplyDelete
  5. mwandishi hivi bao 7 kwa zero siyo habari kwako..ila Azam kufungwa kamoja ni habari na Fei kwenda TP ni habari..kwa taarif yako haendi popote ...hizo ni tetesi....fununu

    ReplyDelete
  6. Huko Mazembe mnataka kumpoteza kama alivyopotea Ramadhan Singano "Mesi". Atafutiwe timu za kaskazini mwa Afrika au hata ligi ndogo za Ulaya lakini huko Mazembe kama hayakumkuta ya kina Ambokile basi yatamkuta ya Thomas ulimwengu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic