November 1, 2020


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa unaamini kwamba una nguvu ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa mara nyingine tena licha ya kuanza kwa kuyumba ndani ya msimu wa 2020/21.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwenye maisha ya soka kuna mapito ya kipekee ambayo wakati mwingine unashindwa kuwa na chaguo kutokana na matokeo ambayo unayapata jambo ambalo linasababisha timu kuyumba kiasi chake.


Kwenye mechi mbili mfululizo zilizopita Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ilikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kuyeyusha pointi sita jumlajumla ndani ya uwanja.


Hali hiyo ilipelekea kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa kumtimua kocha wa makipa Muharami pamoja na aliyekuwa meneja wa timu hiyo kwa wakati hu Patrick Rweyemamu.

Ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na ilinyooshwa ba 1-0 dhidi ya Ruvu Shoting jambo ambalo liliwapa maumivu mashabiki wa Simba pamoja na viongozi kiujumla.


Manara amesema:"Kwenye maisha ya soka kuna matokeo magumu na ya ajabu wakati mwingine ndivyo ambavyo soka lipo lakini hakuna sababu ya kukata tamaa kwa sababu ni nyakati ambazo tunapitia.


"Bado imani yangu ni kwamba kikosi chetu ni imara na tunaweza kutetea taji letu tena kwa msimu wa 2020/21 hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti."


Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 8 ndani ya ligi kinara ni Azam FC mwenye pointi 22.

2 COMMENTS:

  1. Simba ni African champions league team Wachezaji lazima wawe na mentality ya kucheza kila mechi vita yaani kujitoa kwa kila mechi ndio mazoezi yenyewe.Kuna baadhi ya wachezaji wa simba wanaonekana kana kwamba wana mawazo ya kwamba asipocheza vizuri basi atabadilishwa na mchezaji mwengine atakuja kufanya kazi yake.Inakuwaje mchezaji unaesugua benchi unapata nafasi ya kucheza halafu unaendelea kucheza chini hata ya kile kiwango chako mwenyewe cha kawaida wacha hata kile cha mshindani wako wa namba? Nilimuonea huruma sana Cletus chama kwenye mechi ya Mwadui kwani alikuwa anajitoa muhanga kutafuta nafasi za kufunga kwa timu yake ila nafasi hizo mara nyingi zilikuwa zikipotezwa kizembe.Urejeo wa chama ndani ya kikosi cha simba umerejesha amani ndani ya kikosi hicho na kwakweli kila mchezaji wa simba anatakiwa kujituma kama chama au kuliko.Licha ya kipaji ila cletus chama anajituma mno uwanjani huo ndio ukweli.Huwa tunaona hata anapokuwepo nyumbani huwa anaturushia clip za video akifanya mazozi yake binafsi lakini ukisikiliza baadhi ya interview za wachezaji wetu wazawa vipi wanatumia muda wao wakiwa nyumbani mara nyingi husema wanatizama sana t.v. na zile show wanazozipenda kwenye runinga. Kweli kuna maisha baada ya mpira ila professional ya mtu kiuhalisia ndio maisha yake na si vinginevyo kwa mtu mwenye malengo na hana budi ya kuyaishi maisha ya kazi yake. Binaadamu si mashine ila anaefanya nae kazi si mashine pia ni binaadamu mwenzake inapokuaja suala la mchezo wa mpira ni kuzidiana maarifa tu. Kapombe na Shabalala ni beki viungo kasi wa maana ila kama ningepata nafasi ya kuwauma sikio basi ningewaambia jambo moja tu.Nafasi zao sawa na rubani wa ndege anaetaka kutua lazima akihakikishe mazingira yote yapo salama kabla ya kuchukua hatua ya kushusha ndege la sivyo kama hali hairuhusu atajaribu wakati mwengine au hata sehemu nyengine ya kutulia. Nina maana yakwamba usalama ama ulinzi kwanza wa goili na nafasi inapopatikana mtumie kwa uangalifu na umakini mkubwa. Na ndio maana mabeki winga wengi wenye mafanikio wakifanya move ya kwenda kushambulia kama sio goli penalt au hata setup.Ni mawazo binafsi kwani nimeona hawa vijana mara nyingi wanafanya kazi kubwa ya kusadia mashambulizi yasiodhaa matunda ni upotevu wa rasilimali nguvu ndani ya timu.Wawe na uthubutu wa kufunga wao wenywe pia ili kuwapa wakati mgumu mabeki wa timu pinzani kushindwa kubashiri maamuzi yao. Ni wachezaji ninao wakubali sana na ni nafasi peke ndani ya simba zenye uhakika wa kuchezwa na wazawa hivyo wasiridhike na mafanikio walionayo kila kukicha wafikirie kuwa bora zaidi hasa kwenye body fitness iwe ya kujiongeza kila siku.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic