CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hakuna mchezaji wake anayeweza kucheza mechi nne ndani ya siku 12 kutokana na ratiba kuwataka kufanya hivyo jambo ambalo linamlazimu kubadili kikosi mara kwa mara.
Kaze ambaye amesaini dili la miaka miwili amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tatu na ameshinda zote ndani ya uwanja na kusepa na jumla ya pointi tisa.
Alianza kushinda mbele ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru kwa bao 1-0 kisha alishinda mbele ya KMC kwa mabao 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba na jana Oktoba 31 alishinda bao 1-0 dhidi ya Bashara United Uwanja wa Karume, Mara.
Kaze amesema:"Nina mechi nyingi na ngumu ambazo ni lazima wachezaji wapambane na wafanye kazi ngumu ya kusaka ushindi lakini hakuna anayeweza kucheza mechi zote nne mfululizo ndani ya kikosi kwa wakati huu wa kusaka ushindi.
"Ambacho ninakifanya ni kuona kwamba kila mchezaji anacheza na ninawafanyia mabadiliko wachezaji wangu ili kuona kwamba wanaweza kuwa fiti kwa ajili ya mechi zijazo.
"Kikubwa ninachofurahi ni kwamba kila mmoja anaonyesha uwezo wake ndani ya uwanja na anafanya vile ambavyo ninamwambia."
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 22 imecheza mechi 8, imeshinda mechi saba na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons.
Ila Metacha, Mwamnyeto,Lamine, Mukoko,Fei hao ni given lazima waanze
ReplyDelete