November 23, 2020

 


JOHN Bocco, mzawa na mfungaji bora wa muda wote kwa wazawa kibindoni amefikisha jumla ya mabao 130 ndani ya Ligi Kuu Bara akitumika ndani ya timu mbili Bongo.


Ametumia miaka 10 kuparanganyika ndani ya Azam FC ambapo akiwa huko alifanikiwa kuwa mfungaji msumbufu na asiyechoka jambo lililowavutia Simba na kumvuta kikosi cha kwanza.


Akiwa na Azam FC alitupia jumla ya mabao 87 kibindoni yaliyompandisha chati nahodha huyo wa Simba.


Mabao 43 ameyatupia akiwa ndani ya Simba ambayo ameitumikia kwa misimu minne ya soka lake la ushindani.


Mabeki wengi Bongo pamoja na washambuliaji wamekuwa wakimzungumzia Bocco kuwa mchezaji wa mfano ndani ya uwanja pamoja na nje ya uwanja kutokana na nidhamu yake.


Dickson Job, beki chipukizi anayecheza ndani ya Mtibwa Sugar ameweka wazi kuwa katika maisha yake ya soka amekuwa akipiga hesabu ndefu namna ya kukabiliana na mzawa huyo.


"Nimekutana na washambuliaji wengi wenye uwezo ila Bocco ni habari nyingine, hajua kuhusu kukata tamaa wewe mpige mabuti unavyoweza anakutazama kisha anaendelea na majukumu yake unaweza kudhani amekuacha, anakuja tena"

6 COMMENTS:

  1. Ni halali awe mfugaji bora wa muda wote maan hategemei kucheza nje ya ligi ya bongo

    ReplyDelete
  2. Huyo wako aliyekakamaa amefunga magoli mangapi?

    ReplyDelete
  3. Mijitu mingine inajua kuponda tu hata pale penye ukweli ni kuponda mwanzo mwenga. Kama hilo jamaa hapo juu limenikera kumwita Bocco mlegevu, pumbafu kabisa nguchiro wewe. Bocco ni next level hakuna kama yeye bongo hii kwa wazawa.

    ReplyDelete
  4. Mfungaji bora wamuda wrote Tanzania ni hussem masha anagori 154 katika kalia take yampira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic