November 1, 2020

 


HATIMAYE siri imefi chuka kuwa kompyuta mpakato ‘laptop’ aliyokuwa akiitumia mtendaji mmoja wa Simba ndiyo imeonyesha kuwa timu hiyo inahujumiwa na wapinzani wao.

 
Hivi karibuni Klabu ya Simba iliwatimua watendaji wake wanne, lakini haikuweka wazi sababu rasmi zilizochangia kuwatimua watu hao.

 
Simba iliwatimua Meneja Patrick Rweyemamu, Kocha wa Makipa Muharami Mohammed, Ally Shantra na Jacob ambao wapo kitengo cha habari.

 
Timu hiyo imefanya hivyo baada ya kutoka kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye ligi hali iliyozua sintofahamu licha ya kuwa ilifanya usajili mkali kwenye dirisha kubwa lililofungwa Agosti 31, mwaka huu.

Awali, Simba ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Prisons kule Sumbawanga katika Uwanja wa Nelson Mandela kisha ikapokea kichapo kama hicho dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

 
Chnzo cha ndani kutoka Simba kimelieleza Championi Jumamosi kuwa, hujuma hizi zilibainika baada ya mtendaji mmoja aliyeondolewa kwenye timu hiyo kukabidhi kompyuta ya ofi si ambayo alikuwa anaitumia ilikuwa na meseji kadhaa za mtandao wa WhatsApp kuonyesha kuwa alikuwa na mawasiliano na kigogo mmoja wa timu pinzani.

 
“Unajua mara nyingi ukitumia WhatsApp kwenye kompyuta lazima uwe makini sana vinginevyo inaweza kukuumbua.

“Kuna ofi sa mmoja aliondolewa hapa, lakini kwa kuwa alikuwa anatumia kompyuta ya ofi si alitakiwa kuikabidhi na kwa bahati alikuwa hajafunga WhatsApp yake kwenye kompyuta na hivyo meseji zikawa zinaendelea kuingia zikionyesha jinsi ambavyo amekuwa akiwasiliana na kigogo mmoja mkubwa wa wapinzani.



“Meseji zile zilikuwa zinaonyesha jinsi ambavyo kigogo huyo anataka kufahamu baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na kufahamu mambo mengi yanayohusu usajili wa timu na alikuwa anajibiwa na mtendaji huyo lakini pia kulikuwa na meseji za watendaji wengine ambao zilionyesha wakiulizana baadhi ya mambo na mtendaji huyo,” kilisema chanzo hicho.

CHANZO: CHAMPIONI JUMAMOSI

17 COMMENTS:

  1. Bongo Team ikifungwa kila mtu ataonekana nsaliti, ahahahaa

    ReplyDelete
  2. Hizi ni prwopaganda tu, tuache mambo ya kizamani!
    Hivi kuwasiliana Senzo kunamfanya John Boko akose penati au Manula akosee kucheza mpira wa faulo?
    Tuliteleza tukaanguka, tujisahihishe.
    Tupunguze kujiamini kwa kucheza na matokeo "kikosi kipana" kitapanuluwa kweli ohoooo

    ReplyDelete
  3. Ndio mana alifukuzwa huyo senzo fuluzeni na hao wote wenzake waende huko GONGOWAZI

    ReplyDelete
  4. Ahahahah swimba bwana muache kumfukuza chama ambaye hakuwepo mnamfkuza mpishi��������������

    ReplyDelete
  5. inasaidia sana endapo timu inacheza mechi ikiwa na kikosi kamilifu cha first eleven..
    Simba ilipocheza na Tanzania Prison ilikuwa haina wachezaji wake watano walio katika first eleven...hali hiyo ilijirudia pia ilipocheza na Ruvu

    Jana biashara ilikosa wachezaji wake watano pia...
    Hebu fikiria Yanga ikikosa hata wachezaji watatu tu wa first eleven..
    Mwaka juzi ilikuwa hivyo hivyo...ushindi wa kila baada ya dak 70..na waliongoza ligi hadi zikiwa zimebaki mechi nne ligi ikamilike
    Hakuna tofauti ya Zahera,Kaze na kocha waliotimuliwa...matokeo ni yale yale kilichoongezeka ni umiliki wa mpira tu!

    ReplyDelete
  6. Hizo message ndo zilicheza mpira au? onesha palipo na hujuma exactly watu waelewe. Manara mbona mara kibao anaongea na watu wa timu pinzani? hujuma kivipi zilizo directly na corelarion influence ndani ya uwanja. PROPAGANDA MWANDISHI NA WAHARIRI

    ReplyDelete
  7. Habari ya kijinga hii. Ina maana Simba au Yanga hazipaswi kufungwa kwenye hii ligi inayoendelea? Kwanini hamtaki kuheshimu uwezo wa timu nyingine zaidi ya Simba na Yanga? Real Madrid imefungwa na timu iliyopanda daraja msimu huu Cadiz je nayo ni hujuma? Bsi tusiwe na ligi Simba na Yanga pekee wawe wanacheza wenyewe kwa wenyewe na anayeshinda apewe ubingwa maana ndio wenye haki ya kuzifunga timu nyingine. Hizi ni habari za kuuzia magazeti tu ili uweze kutumia whatsapp kwenye Computa inabidi uwe na Simu karibu na unascan indipo unatumia sasa ikiwa kaondoka na simu yake hizo whatsapp kwenye computa zimefungukaje au na simu yake aliwaachia?

    ReplyDelete
  8. kufungwa mechi mbili mmeanza kumtafuta mchawi sasa bado tar 7 mtamfukuza mpaka mzee wa billion 20

    ReplyDelete
  9. Timu bila chama hakuna kitu tumeligundua hilo kwahi kazi mnayo hapo mikia fc

    ReplyDelete
  10. Simba akili wameuza wanatembea na fuvu tu

    ReplyDelete
  11. umesema mawasiliano yslikuwa wanazungumzia usajili usajili unahusika vp na kiwanjan?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic