BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck huenda atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Coastal Union Novemba 21, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Tayari kikosi cha Simba kimetia timu Arusha ambapo kilianza safari ya kuwafuata wapinzani wake Novemba 19 jioni na kuwasili salama jijini Arusha.
Morrison alikuwa nje kuitumikia adhabu ya mechi tatu pamoja na faini ya laki tano, (500,000) baada ya kumpiga ngumi beki wa Ruvu Shooting, Juma Nyosso na wote wawili walikumbwa na adhabu hiyo iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Bara.
Jambo hilo lilikuwa Uwanja wa Uhuru wakati Simba ikichezeshwa mpira gwaride na kufungwa bao 1-0 na kuyeyusha jumla pointi tatu.
Nyota huyo ambaye ni mashine mpya ndani ya Simba baada ya kuibukia huko akitokea kwa watani wa jadi, Yanga alikosa mechi tatu ilikuwa mbele ya Mwadui FC na Simba ilishinda kwa mabao 5-0,Simba 2-0 Kagera na ule wa dabi dhidi ya Yanga uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imecheza mechi 10 na kufunga mabao 22, yeye amehusika kwenye bao moja kwa kutoa pasi moja ya bao.
0 COMMENTS:
Post a Comment