NYOTA watatu wa kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wanatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Azam FC ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 itakutana na KMC iliyo nafasi ya sita na pointi 15.
Kwa mujibu wa Vivien Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa maandalizi yapo sawa ila watawakosa wachezaji watatu kwenye mchezo huo.
Nyota hao ni Salim Abubakar,'Sure Boy' ambaye aliumia akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Frank Domayo ambaye aliumia mazoezini pamoja na Oscar Masai ambaye aliumia muda mrefu.
Mchezo huo utachezwa saa 10:00 jioni unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zimeanza msimu wa 2020/21 kwa kasi.
KMC iliweza kufanya vema kwenye mizunguko mitatu ya mwanzo ambapo ilifanikiwa kuongoza ligi jambo ambalo wanalipigia hesabu kwenye raudi za wakati huu kuku Azam FC ikihitaji kuendeleza rekodi ya kukaa namba moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment