KIKOSI cha Tanzania Prisons leo Novemba 20 kimelazimisha sare ya bila kufungana na timu ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.
Mpaka dakika 90 zinakamilika kwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa Ludovick Charlse ambaye aliweza kuumudu mchezo wa leo hakuweza kuwaita wachezaji kati kuanzisha mpira ndani ya kipindi cha kwanza na cha pili.
Shukrani kwa Abobakary Mshery mlinda mlango wa Mtibwa Sugar ambaye alikuwa nguzo imara kwenye lango baada ya kuokoa hatari tatu za moto zilizokuwa zikielekea kwenye lango lake.
Mtibwa Sugar hawakuwa na presha kubwa ya ushambuliaji kwenye mchezo wa leo jambo lililomfanya mlinda mlango, Jeremia Kisubi kuwa salama kwa muda mrefu.
Baraka Majogoro, kiungo wa Mtibwa Sugar hakuachwa salama ndani ya dakika 90 alikutana na adhabu ya kadi ya njano baada ya kuonekana akiunawa kwa makusudi mpira wakati wa harakati za kuokoa mpira akiwa nje kidogo ya 18.
Godfrey Luseke naye wa Mtibwa Sugar alikutana na kadi ya njano huku kwa Tanzania Prisons, Samson Mbangula ambaye aliingia uwanjani dakika ya 38 akichukua nafasi ya Salum Bosco alipewa zawadi ya kadi ya njano.
Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar kufikisha jumla ya pointi 12 kibindoni huku Tanzania Prisons ikifikisha jumla ya pointi 16 zote zikiwa zimecheza mechi 11.
0 COMMENTS:
Post a Comment