IMEBAINIKA kuwa Klabu ya Azam FC imeingilia dili la kiungo Issa Ndala wa Plateau United mwenye uraia wa Nigeria ambaye anahusishwa kujiunga na Yanga kupitia dirisha hili dogo la usajili.
Ndala ambaye anacheza katika sehemu zote za kiungo wa kati yaani kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji amekuwa gumzo hapa nchini kutokana na kuonyesha kiwango katika mchezo dhidi ya Simba ambao ulikuwa wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezaji huyo amesema kuwa, ukiachana na Yanga ambao wapo kwenye maongezi nae pia klabu ya Azam imemtafuta kuulizia masuala ya usajili wake wa kujiunga na timu hiyo.
"Nimekuwa nikizungumza na Yanga ambao wao ndio walikuwa wa kwanza kunitafuta mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Simba wakati nilipokuja huko Tanzania.
"Ukiachana na Yanga kuna timu pia inaitwa Azam ambao viongozi wao wamenitafuta kwa ajili ya mazungumzo wakiwa wanahitaji huduma yangu.
"Mpaka sasa hatujakubaliana na timu yoyote ila timu zote zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yangu, kwa sasa ni ngumu kusema kuwa nitaenda wapi kati ya Yanga na Azam lakini nipo tayari kucheza soka nchini Tanzania kama kutakuwa na dili zuri la usajili,” amesema mchezaji huyo.
Chanzo:Championi
Happy utasikia huyo jamaa wa Azam mala tumewazidi kete Yanga ,endelea kuwaingiza Chaka
ReplyDeleteMambo ya kupandishiana dau tuu
ReplyDeleteAlly Niyonzima anafanya nini cha maana pale Azam ulivyokuwa unashabikia Yanga walizidiwa kete na Azam?
ReplyDelete