December 14, 2020

 


GERARD Houllier, aliyekuwa kocha wa zamani wa Klabu ya Liverpool ametangulia mbele za haki akiwa na umri wa miaka 73 na ujumbe wake wa mwisho alisema kuwa atapambana kurejea katika hali ya kawaida.

Houllier ambaye pia amewahi kuifundisha Klabu ya PSG, Aston Villa na Lyon alifanyiwa upasuaji hivi karibuni.

Amekuwa kwenye stori ndefu juu ya matibabu yake kwa kuwa alikuwa akitumia dawa na inatajwa kwamba tatizo la presha limesababisha kifo chake.

Alikiongoza kikosi cha Liverpool msimu wa 2001 ametajwa na wachezaji wa zamani kwamba ni miongoni mwa makocha bora wenye uwezo wa kufundisha kwa umakini.

Raia huyo wa Ufarasa ametangazwa pia kupitia vituo vya radio nchini humo ambapo kupitia RMC na magazeti ya Habari za Michezo L'Equire zimeripoti kwamba kocha huyo amefariki baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo Paris.

Kupitia kwa Vincent Duluc,aliripoti kwamba Houllier alifanyiwa upasuaji wiki tatu zilizopita na alirejea nyumbani Jumapili. 


Ameripoti ujumbe uliotumwa uliandikwa:"Ninapambana kwa sasa lakini ninadhani nitatoka katika hili,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic