December 20, 2020


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa nyota wake Alain Thiery Akono Akono amepata dili la kwenda Malysia baada ya mabosi wa timu hiyo kuvutiwa na uwezo wake.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabiti amesema kuwa kila kitu kikiwa wazi ataweka sawa na mashabiki watajua ni timu ipi anakwenda.


Akono anakuwa ni nyota wa tatu kusepa ndani ya kikosi cha Azam FC na kuibukia kwenye timu nyingine kupata changamoto mpya.

"Mazungumzo na kila kitu kuhusu usajili wa Ankono Akono yamekwenda sawa na kinachotakiwa ni mashabiki kuwa na subira ili kupata taarifa kamili ambazo tutazitoa hivi karibuni, ila ukweli ni kwamba amepata timu Malysia" .


Akono anakuwa ni mchezaji wa tatu kuuzwa kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Klabu ya Azam FC wengine ni pamoja na Novartus Dismas ambaye yupo Israel na Shaban Chilunda yupo zake nchini Morroco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic