December 18, 2020

 


RASMI, Deogratius Munish msimu wa 2020/21 atakuwa ni mali ya Klabu ya Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Nyota huyo ameibuka ndani ya Ihefu FC inayopambana kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Klabu ya Lipuli FC msimu uliopita iliposhuka daraja na sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Munish wengi wanapenda kumuita Dida aliwahi kuwa kipa namba moja ndani ya Klabu ya Yanga na pia alikuwa ni kipa namba mbili wa Klabu ya Simba.


Katwila amesema kwamba lengo la kusajili wachezaji wenye uzoefu na Ligi Kuu Bara ni kuongeza hali ya kujiamini na kupambana kwa vijana wake kwenye mechi zote zilizobaki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic