December 14, 2020


AZAM FC leo imegawana pointi mojamoja na Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mabao ya Azam FC yote yamefungwa na Idd Naldo dakika ya 19 na lile la pili alipachika dakika ya 74.

Namungo FC iliweka usawa dakika ya 25 kupitia kwa Edward Manyama na lile la usiku lilipachikwa na Stephen Sey dakika 90+5.


Hii inakuwa ni mechi ya tatu kwa Azam FC kukutana na Namungo ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 ambapo msimu uliopita mchezo wa kwanza Azam FC ilishinda kwa mabao 2-1 na mchezo wa marudiio Namungo ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Majaliwa.

Jumla zikiwa zimekutana mara tatu yamefungwa mabao nane ambapo kila timu imefunga mabao manne.

Ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, George Lwandamina kukaa benchi anashuhudia vijana wake wakianza kwa sare na kufanya ifikishe jumla ya pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu na Namungo inafikisha jumla ya pointi 17 ikiwa nafasi ya 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic