SHUJAA wa soka, ikiwemo mafanikio yake katika Kombe la Dunia 1986 alipofunga bao la ‘Mkono wa Mungu’ dhidi ya England, atazidi kukumbukwa lakini upande wa pili familia yake inaweza kumkumbuka tofauti.
Huyo ni Diego Mara dona ambaye alifariki wiki kadhaa zilizopita ameacha vita kubwa ya urithi wa mali zake hasa kwa watoto.
Inaelezwa kuwa licha ya watoto sita ambao wanajulikana bado kuna wengine ambao wameibuka na kuruhusu mgawanyo wa mali za Maradona ambao umeanza kuwa tatizo
Inaelezwa kuwa Maradona ameacha utajiri wenye thamani ya pauni 37m na katika waraka aliouandika wa jinsi mali zake zitakavyo gawanywa hapo ndipo kumeibuka na kizaazaa.
Watoto wanao julikana na wengi kuwa ni wa staa huyo ni watano, lakini kuna mwingine ameibuka, kuna dada zake wanne na wapenzi wake na wake zake wa zamani nao wametajwa kutaka kuwemo katika urithi huo.
Wanasheria wa familia ya Maradona wanatarajiwa kuanza kuingia katika vita ya mgawanyo wa mali kwa kuwa wapo ambao wanaona walistahili kupata nyingi au kiasi kikubwa kuliko wengine na wapo wanaoona kuwa wote wanatakiwa kupewa mgao sawa kama marehemu mwenyewe alivyotaka iwe.
Watoto maarufu wa nguli huo, Dalma, 33, na Giannina, 31, wamekuja juu na kumshutumu mwanasheria wa Maradona, Matias Morla, ambaye ndiye aliyeweka wazi juu ya waraka wa Maradona aliouandika mwaka 2012, wakidai kuwa anahusika katika mambo mbalimbali ya ‘kipuuzi’ kuhusu urithi wa baba yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment