KIKOSI cha Azam FC leo Desemba 14 kinatarajia kusaka pointi tatu dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Azam Complex huku kikikosa huduma za nyota wake watatu ambao wamehusika kwenye mabao 12 kati ya 19.
Msimu uliopita Azam FC ilitolewa kwenye reli ya kusaka ubingwa na Namungo FC baada ya kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Majaliwa. Namungo pia haijawahi kushinda Azam Complex ilifungwa mabao 2-1 walipokutana kwenye mchezo wa ligi msimu uliopita.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kwamba nyota watatu watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Prince Dube, Salum Abubakar. ‘Sure Boy’ na Abdalah Kheri.
Sure boy mwenye pasi moja na bao moja ndani ya Azam FC aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United, Abdalah Kheri aliumia kwenye mchezo dhidi ya Gwambina.
Prince Dube mshambuliaji wa kikosi hicho mwenye mabao sita na pasi nne za mabao aliumia kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 14 ndani ya Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment