December 31, 2020


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa hana tatizo na mshambuliaji namba moja wa kikosi hicho Meddie Kagere.

Imekuwa ikielezwa kuwa Sven na Kagere hawaivi chungu kimoja jambo ambalo lilikuwa likimfanya amsotesha benchi nyota huyo ndani ya kikosi cha Simba.

Tayari kwa sasa ameanza kumtumia nyota huyo ambaye ametupia jumla ya mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

Jana, Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Ihefu FC alitupia mabao mawili na kutimiza majukumu yake ndani ya uwanja.

Sven amesema:"Sijui haya aneno huwa yanatoka wapi ila ninachojua mimi ni kwamba kila mchezaji ndani ya kikosi cha Simba ni muhimu na wote ninafanya nao mazungumzo.


“Wachezaji wangu kwa asilimia kubwa wanapambana na sitaki kuona kwamba wanakuwa wanakosolewa kwa namna yoyote ile. Lawama zao zote lazima zije kwangu na isiwe kwao.


"Sina ugomvi na mchezaji na siwezi kumhukumu kwa masuala ya nje ya uwanja mimi ninachohitaji ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu ndani ya uwanja," .




10 COMMENTS:

  1. Mwandishi acha usenge wa kutengeneza habari yenye lengo la kuvuruga simba, wewe kama umetumwa wahi gsm kachukue hela yako ila lengo lango hutafanikiwa. Hiyo habari uliivumisha kipindi kile ikapita bila mafanikio ya nini tena leo unairudisha humu? Acheni upuuzi bwana

    ReplyDelete
  2. Umeshindwa kuandika habari za mechi ya leo unataka kutuhamishia kule tena? Hata kama mnalipwa tumieni hata akili kidogo mliyonayo kubalance stories wapuuzi ninyi

    ReplyDelete
  3. Wameona kagere ameanza kufunga uoga umeanza ndio maana wanafufua habari za kijinga

    ReplyDelete
  4. Makanjanja wanalipwa kwa kuandika uzushi na ujinga.Nenda GSM ukapewe bahasha yako.

    ReplyDelete
  5. Mwandishi huyu pumbu kweli,badala aelezee mechi zenye znaendelea na mapungufu yake,anatuletea stori za kikuda

    ReplyDelete
  6. Nagikiri ni huyo ndie alieandika kuwa Kagere keshapokea mkwanja makubwa kutoka yanga kwa kuhamia huko na pia Chama ni kati ya wachezaji 25 wa kigeni anaowatangaza kuhamia yanga

    ReplyDelete
  7. Sijui kwa nini waandishi wengi humu wana mambo ya kipumbuwavu sana

    ReplyDelete
  8. Hajaandika utumbo wao walio bahatosha hilo goli la kufosi vyura huyu na hao kandambili wenzake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wandishi Tz hawana elimu mradi ujuwe kuandika na kusona basi unakuwa muandishi. Na kibaya zaidi hawajuwi kuwa wasomaji wao wanaupeo mkubwa kuliko wao

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic