TANZANIA Prisons ikiwa Uwanja wa Nelson Mandela imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wa mzunguko wa pili.
Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilitoshana nguvu bila kufungana ndani ya dakika 45 za mwanzo za mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Kipindi cha pili,Prisons walianza kupata bao dakika ya 52 kupitia kwa Jumanne Elifadhili.
Bao la kuweka usawa kwa Yanga lilifungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 76 katika harakati za kuweka mzani sawa ndani ya uwanja.
Yanga imefunga mwaka 2020 ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 vila kupoteza na kugawana pointi mojamoja na Prisons.
Hili linakuwa ni bao la pili kwa Ntibanzokiza ambaye ni ingizo jipya, bao lake la kwanza alifunga mbele ya Dodoma Jiji.
Sare hiyo inaifanya Yanga kufikisha pointi 44 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 18, Tanzania Prisons inafikisha pointi 22 ikiwa nafasi ya 9.
Kila mtu ashinde mechi zake hatutasikia tena.Mambo yameanza kuwa magumu.Ligi ni marathon sio sprint.
ReplyDeleteNyie si mlikung'utwa?
DeleteNa kila mtu afungwe mechi zake
DeleteFikiria endapo Yanga leo isingekuwa na wachezaji wake watano wa kikosi cha Kwanza, yaani Lamine,Saido, Sarpong, Tuisila na Mukoko..Ndiyo ilikuwa hivyo kwa Simba..Kikosi cha Yanga ni hicho hicho..iwe ihefu au polisi hata Azam
DeleteIle kauli ya "Tuna kikosi kipana" imeyeyukia wapi?
DeleteBADO IPO SI UMEONA HAKUNA WAWA WALA MKUDE NANYONI IHEFU KALIWA 4.
DeleteInategemeana lakin chama si alikuwepo baba yenu na uwanja haukuwa na tope Kama leo
DeleteKwahiyo ninyi mnacheza kiangazi tu
DeleteLeo vipi mliogopa kutupa taarifa wakati mechi inaaendelea au tatizo nini?
ReplyDeletePakua azam max hauitaj hata kuwekewa live updates
DeleteThe time will tell,tusubiri.
ReplyDeleteHata mimi nilishangaa hapakuwa na live updates, labda masharti ya mganga
ReplyDeleteInawezekana maana uto wanaamini Sana hizo Mambo, leo kila Mara walikuwa wanafukua kwenye goli la prison
DeleteMtakeleka ha2japoteza mchezo litawachoma sana na ha2fungwi mlijua 2tafungwa ha2fungwi subirini mwakan 2wape dozi mikia nyie
ReplyDeleteTatizo kipindi hiki ni masika na nyani hamuwezi kucheza kwenye uwanja uliyolowa maji, sijuwi mtafanyaje!!!
DeleteWakipenda wakichukia, wakiandika wasiandike mnyama ana close in, anapiga hodi na milango imeshafunguliwa
ReplyDeleteNguruwe fc mbona mnajifanya kuteseka hivi, au kisa mlibanjuliwa
ReplyDelete