KIUNGO mkabaji wa Klabu ya Yanga Abdulaziz Makame yupo kwenye mpango wa kutua kwa mkopo ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania.
Habari zinaeleza kuwa mpaka sasa ni timu mbili zinahitaji kupata huduma yake ikiwa ni Polisi Tanzania na Ihefu.
Sababu kubwa ya nyota huyo mzawa kuondoka ndani ya Yanga ni kukosa nafasi kikosi cha kwanza licha ya uwezo alionao.
Yanga ipo Arusha ambapo itacheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji na nyota huyo hayupo kwenye kikosi.
Kocha Mkuu, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji ambao hawatumii bado wameshindwa kuonyesha uwezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment