KIUNGO mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba, Miraj Athuman huenda akaibukia ndani ya Namungo FC kwenye usajili wa dirisha dogo.
Nyota huyo ambaye msimu uliopita alitupia mabao saba na pasi moja ya bao msimu huu amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Habari zinaeleza kuwa miongoni wa timu ambazo zinahitaji huduma yake ni pamoja na Namungo FC na Ihefu FC kwa mkopo.
Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuber Katwila amesema kuwa mpango wa timu hiyo kwa sasa ni kuboresha kikosi hicho ili kuwa bora kwenye mechi zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment