December 16, 2020


HUENDA Tuisila Kisinda Kiungo wa Klabu ya Yanga akawa fiti kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya kupatiwa matibabu.

 

Kiungo huyo alishindwa kumalizia mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC baada ya kupata majeraha ya goti yaliyosababisha ashindwe kuendelea na mchezo huo.

 

Yanga katika mchezo huo walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 5-0 kati ya hayo moja alilifunge yeye Tuisila kwa shuti kabla ya kuumia na kutolewa nje kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Daktari Mkuu wa timu hiyo, Shecky Mgazija amesema kuwa mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu, kwani mchezaji wao Tuisila yupo fiti kwa ajili ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.


“Ninafahamu mashabiki wengi wa Yanga wanataka kufahamu maendeleo ya Tuisila, kwa kifupi ni kuwa anaendelea vizuri baada ya kumpatia matibabu ya haraka pale uwanjani.

 

“Majeraha yenyewe aliyoyapata siyo makubwa sana, zaidi alipata mshtuko kwenye sehemu ya goti, hivi sasa anaendelea vizuri baada ya matibabu ya haraka tuliyompatia.

 

“Hivyo, huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachocheza na Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi wiki hii, hivyo mashabiki waondoe hofu kwenye hilo mchezaji wao yupo fiti kabisa,” amesema Mgazija.


Yanga itamenyana na Dodoma Jiji, Desemba 19 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic