KOCHA wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery amesema kuwa timu aliyopo kwa sasa ina historia kubwa na anaamini kwamba itarejea kwenye ubora.
Thiery amechukua mikoba ya Zuber Katwila ambaye ameibukia ndani ya Ihefu baada ya kubwaga manyanga ndani ya kikosi hicho.
Pia timu yake ya zamani ya Namungo ambayo alikuwa anaifundisha Thiery ipo chini ya Hemed Morroco.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema:"Nipo huku na maisha yanakwenda kwani kazi ni kazi kikubwa ni kufanya kwa juhudi.
"Unapozungumzia Mtibwa Sugar ni moja ya timu kubwa na bora hivyo bado tunapambana kufanya vizuri," .
0 COMMENTS:
Post a Comment