December 29, 2020


AMRI Kiemba, kiungo aliyecheza kwa mafanikio ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kabla ya hivi karibuni kuamua kutundika daluga amesema kuwa suala la Bernard Morrison kuchanga ili kesi yake isikilizwe halimuingii akilini.

Kiemba pia amewahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba, Yanga na Ruvu Shooting na kote alikuwa ni chaguo la kwanza la walimu aliokuwa akifundishwa nao.

Kwa sasa Kiemba anasimamia kituo cha kukuza vipaji kwa watoto kilichopo Mabibo, Dar.

Nyota huyo amesema kuwa sakata la Morrison kwa uelewa wake kwenye suala la mchezaji huyo kutakiwa pia kulipa faini ili kesi yake isikilizwe halimuingii akilini.


"Kwa ufahamu wangu mdogo kwa mambo ya kesi linapokuja ishu ya kulipia anayepaswa kulipa ni yule anayekwenda kushtaki na siyo mshatikwa.

"Anayeshtaki ndiye anapaswa kulipa masuala ya kesi sasa kwa namna ilivyo kwamba anayeshtakiwa naye anatakiwa kulipa bado hainiingii akilini," .

Morrison anashtakiwa na Yanga kuhusu sakata lake la mkataba wake ambapo yeye anadai kwamba alisajiliwa kwa muda wa miezi sita ndani ya Yanga.

Yanga ambao wanamshtaki wanadai kwamba ana dili la miaka miwili hivyo bado ni mchezaji wao halali ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Cedric Kaze.

Hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliweka wazi kwamba wameambiwa na mahakama ya usuluhishi,(Cas) kwamba wanatakiwa kulipa fedha wote wawili, mchezaji na wao ili kesi yao isikilizwe.


14 COMMENTS:

  1. Manyani ndo yanadanganywa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni mbwa usiyejjijua aliyewatukana Yanga ni Mzungu ambao ndio wanaendeleza ubaguzi wa rangi kote duniani na wewe unajifira mwenyewe kwa kudhani unawatukana yanga. Kweli bongonyoko ni bongonyoko maruni...

      Delete
  2. Nutakuwa mtu wa mwisho kuamini suala hilo. Yanga wanawachezea mashabiki wao. Hakuna kesi wala nini

    ReplyDelete
  3. Hakuna kesi ya hivyo Utopolo hawana jambo

    ReplyDelete
  4. Kwenye arbitration case mnalipa pande zote, Mwakalebela is right

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwenye mkataba wao kulikuwa na kipengele cha arbitration?

      Delete
  5. Nacheeka, waafrika wanajitukana wenyewe, ilihali mzungu?

    ReplyDelete
  6. nyie waandishi ni sawa mavi ya chooni kabisa

    ReplyDelete
  7. Hiyo siyo Mahakama ya Jinai au madai hiyo Mahakama ya Usuluhishi na inataratibu zake, hii ndiyo mara ya kwanza kwa Bongo mgogoro wake kusikilizwa, asijifanye anajua wakati taratibu zipo hivyo. Hizo ni sheria za CAS....

    ReplyDelete
  8. Hiyo siyo Mahakama ya Jinai au madai hiyo Mahakama ya Usuluhishi na inataratibu zake, hii ndiyo mara ya kwanza kwa Bongo mgogoro wake kusikilizwa, asijifanye anajua wakati taratibu zipo hivyo. Hizo ni sheria za CAS....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic