December 23, 2020

 


MSHAMBULIAJI mzawa Paul Nonga, nyota wa Gwambina FC anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga bao la mapema zaidi ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Nonga ni ingizo jipya ndani ya Gwambina ambapo kwenye usajili wake wa msimu huu ilibaki kidogo atue ndani ya Namungo FC ila dau alilowekewa ndani ya Gwambina lilimvuta.

Aliibuka huko Gwambina akaitokea Klabu ya Lipuli FC ambayo kwa sasa imeshuka daraja inapambana kurudi Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Alifunga bao hilo sekunde ya 33 kwa pasi ya Abdalah Kibadeni wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons,  Uwanja wa Gwambina Complex.

Nonga amesema kuwa ni furaha kwake kufunga na anaamini atazidi kufanya vizuri zaidi na zaidi ili kuipa mafanikio timu yake.


Gwambina FC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza jumla ya mechi 16 ndani ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic