November 13, 2020


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa nyota wao Idd Chilunda alibadilisha timu ya awali aliyotakiwa kujiunga nayo kwa kuwa kocha wa timu hiyo alimkataa.


Chilunda ambaye ni mzawa kwa sasa amejiunga na Klabu ya Moghreb Atletico Tetuan ambapo awali alitajwa kumalizana na Klabu ya Mouloudia zote za Morocco.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa Chilunda alilazimika kuibukia timu nyingine baada ya kocha wa timu ya mwanzo kumkataa.


"Chilunda alitoka Tanzania ili kujiunga na Klabu ya Mouloudia d'Oujda ya Morocco lakini kocha aliyekuwa akimhitaji Abdelhak Benchika alibadilishwa na kuletwa Abdeslam Ouaddou ambaye hakumtaka Chilunda.


"Kutokana na hali hiyo wakala wa Chilunda aliamua kufanya mazungumzo na timu nyingine ambapo alipata timu hiyo ya Atletico Tetuan ambayo imemsajili," amesema.


Chilunda aliwahi kucheza Tenerife ya Hisapnia ambapo hakuweza kuwika sana na kurejea ndani ya Azam FC.

1 COMMENTS:

  1. Hata hpo alipoenda kongore kwake, safari Ni mdogomdogo atafikia mbali tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic