December 30, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa suala la kiungo wa Simba, Jonas Mkude litatolewa ufafanuzi wiki ijayo na kuwataka mashabiki watulie.


Mkude alisimamishwa na Simba Desemba 28 kwa kile kilichoelezwa kwamba ni utovu wa nidhamu na anafanyiwa uchunguzi na Kamati ya Nidhamu ambayo itatoa hukumu yake hivi karibuni.


Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Ihefu FC wakati Simba ikishinda mabao 4-0 hakuwa sehemu ya kikosi cha Sven Vandenbroeck.


Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa suala hilo linafanyiwa uchunguzi na majibu yatatolewa.


"Mashabiki wasiwe na mashaka suala la Jonas Mkude lipo kwenye kamati ya nidhamu litatolewa wiki ijayo, mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kitakwenda sawa," amesema.

8 COMMENTS:

  1. Ss huyu si yule alietongozwa na kuombwa ( ) ni mkude? Ss yy atakua vp shahidi kwa suala hilo? Kibaya zaid alipotongozwa na kuombwa alikua kavaa hivohvo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulikuwepo kipindi anamtongoza ? au nyie ni wale Domo kaya ?

      Delete
  2. Ss huyu si yule alietongozwa na kuombwa ( ) ni mkude? Ss yy atakua vp shahidi kwa suala hilo? Kibaya zaid alipotongozwa na kuombwa alikua kavaa hivohvo

    ReplyDelete
  3. Akitongozwa mtoto wa mwanamke mwenzako usisite kusema. Inaelekea ukuwadi ni kazi yako. Kubwa jinga.

    ReplyDelete
  4. Kuna watu wajinga kweli duniani, hasa kutokea upande ule. Hivi mkude kutuhumiwa utovu wa nidhamu kaanza leo? Hata timu ya taifa alitolewa tuseme alimtongoza nani? Hata kipindi ceo senzo alisimamishea au ndio alimtongoza senzo? Acheni ujinga wa kudhalilisha watu kisa mnalipwa, wapuuzi wakubwa nyinyi

    ReplyDelete
  5. Acha ujinga wewe akili kama vyura mchukuweni nyinyi mnae fanana akili walevi wezenu kandambili aka vyura matopeni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic