December 30, 2020


 KIKOSI cha Yanga leo Desemba 30 kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.


Ni mchezo wa kwanza nzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.


Langoni alikaa Farouk Shikalo kipa namba mbili na Yanga na alitunguliwa na Lambart Sabiyanka na lile la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong. 


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu. 


"Wachezaji wapo tayari na kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu ndani ya uwanja," .

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic