January 7, 2021


HONGERA kwa wawakilishi wetu kimataifa ambao wameanza vizuri ndani ya mwaka 202i kwa kupata matokeo chanya kwenye mechi zao ambazo wamecheza.

Kwa familia ya michezo kila mmoja anatambua namna timu yake ilivyofungwa mwaka 2020 ndani ya uwanja kwa namna ya kipekee baada ya dakika 90 kukamilika.


Zipo ambazo zilimaliza mwaka kwa kupoteza mechi zao na zipo pia ambazo ziliambulia sare na nyingine ziliambulia ushindi baada ya dakika za uwanjani kukamilika.


Yote yanawezekana na kwenye ulimwengu wa mpira matokeo yote matatu yanaihusu timu moja inayoshindana. Ili ushindane ni lazima ukubali kushindwa, kushinda na kutoshana nguvu.


Bado maisha ya soka lazima yaendelee na ushindani pia unapaswa kuedelea kuwa mkali bila kupungua ndani ya ardhi ya Bongo baada ya mwaka 2020 kufungwa.


Kwa wale ambao mipango yao ilikwenda kombo mwaka uliopita ni muda wa kuanza kupanga tena kwa wakati huu ambao ukurasa mpya unazidi kufunguliwa ndani ya masuala ya michezo.


Jambo la msingi ni kuanza kujipanga kwa ajili ya mwaka mpya 2021 kuweza kuweka mambo sawa na kuomba Mungu azidi kutulinda katika yale ambayo tunayapanga.


Ipo wazi kwamba ni kwa neema ya Mungu tupo hapa wakati huu na tunaendelea kupambana kusaka yale ambayo tunaamini ni mafanikio kwenye ulimwengu wa soka.


Kwa upande wa Ligi Kuu Bara ambayo imekuwa na ushindani mkubwa kwa sasa ni mapumziko mafupi ambayo yanaendelea.


Hii inatokana na uwepo wa Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar pamoja na mwendelezo wa mechi za Kombe la Shirikisho.


Kwa Ligi ya Wanawake Tanzania wenyewe bado wanaendelea kujipanga ambapo inatarajiwa kuendelea tena baada ya kupisha zile sherehe za mwisho wa mwaka 2020, kesho Januari 8.


Ligi hii pia nayo mwaka huu mpya 2021 inapaswa ipewe sapoti kwa kuwa imekuwa ikikumbwa na matatizo ya hapa na pale hasa kwa upande wa masuala ya uchumi kwa timu zetu shiriki.


Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) linapaswa lijipange sawasawa ndani ya 2021 kulidhibiti hili kwani kwa kuendelea kuwekeza nguvu zaidi katika soka la Wanawake.


Ikiwa timu 12 zinazoshiriki ligi zikapata sapoti kutoka kwa wadau mbalimbali itaongeza nguvu ya ushindani na kufanya bingwa kuwa na nguvu ya kushindana pia kwenye mechi za kimataifa ikitokea nafasi.


Mwaka huu pia ni mwanzo wa wawakilishi wetu kukamilisha ndoto zao za kukata tiketi ya kusonga mbele kwenye mashindano ya kimataifa.


Kikubwa ni kwamba kwa wakati ujao ni kuangalia namna gani wawakilishi wetu wanaweza kuwa bora na kushinda mechi zao za mwanzo ili kupata matokeo chanya.


Kwa kufanya vizuri ni muhimu ili kupata ushindi katika mechi za kimataifa. Namungo mchezo wa kwanza ilishinda mabao 2-0 dhidi ya El  Hilal Obeid ya Sudani.

Mechi ya kwanza Namungo ilishinda ikiwa nyumbani na ugenini Uwanja wa Al Hilal iliweza kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3.

Ushindi huo unaifanya Namungo kutinga hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho.


Kila mchezahi  akubali kujitoa kwa ajili ya timu na afanyekazi kwa juhudi akiwa uwanjani bila kujali anacheza na nani uwanjani.Ni faida kwa timu na taifa pia.

Mpira ni biashara na ili ufanikiwe kibiashara ni lazima ushindane hata ukiwa ugenini ni lazima ushindane kwa hali na mali kusaka matokeo ndani ya uwanja.

Simba pia mbele ya FC Platinum haikuwa kazi nyepesi kupata matokeo ikiwa baada ya War In Dar kujibu kwa ushindi wa mabao 4-0.


Kila la kheri katika hatua za mbele mipango na upambanaji bado unatakiwa kuendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic