KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amesema uwepo wa beki mkongwe, Kelvin Yondani kwenye kikosi chake, umeongeza umakini kwenye safu yake ya ulinzi.
Polisi Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya nne ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC, Yondani pia alikuwa miongoni mwa kikosi hicho.
Malale amesema: “Kuwa na mchezaji mzoefu kama Yondani kwenye kikosi ni jambo zuri kwani ni mchezaji ambaye amecheza kwa kiwango cha juu kwenye timu kubwa, hivyo uzoefu wake utakuwa msaada mkubwa kwetu kutokana na kikosi chetu kuwa na idadi kubwa ya vijana.
"Tulikuwa na tatizo kwenye safu yetu ya ulinzi jambo ambalo lilipelekea tuwe tunaruhusu mabao mepesi kwenye mechi zetu, hivyo uwepo wa Yondani kikosini kwa kiasi kikubwa utaongeza umakini kweye safu ya ulinzi kutokana na uzoefu alionao.”
Yondani amejiunga na Polisi Tanzania akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kuisha msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment