January 27, 2021

 


LEO Januari 27 Yanga wametambulisha wafanyakazi wawili ambao wanaingia jumla kwenye benchi la ufundi kuendeleza gurudumu la kusaka ushindi ndani ya uwanja.

Miongoni mwa wale ambao wametambulishwa leo ni pamoja na mzawa, Nizar Khalfani ambaye yeye anakuja kuwa kocha msaidizi akichukua mikoba ya Juma Mwambusi ambaye aliomba kujiweka kando kutokana na matatizo ya afya.

Khalfan ambaye ni mchezaji wa zamani wa kikosi cha Mtibwa Sugar alikuwa anaifundisha timu ya African Lyon ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mwingine ambaye ametambulishwa ndani ya benchi la ufundi ni Edem Mortotsi ambaye ni raia wa Ghana yeye anakuja kuwa kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha wa viungo.

Ofisa Uhamasishaji wa kikosi cha Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa malengo ya kufanya hivyo ni kuongoze nguvu ndani ya timu hiyo ya Wananchi.

Wanaungana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic