CHRIS Mugalu, mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Sven Vandenbroeck, amempoteza nyota wa Yanga, Michael Sarpong kwenye suala la kutupuia mabao ndani ya muda mfupi.
Mugalu akiwa amejiunga na Simba msimu huu, ametumia muda mchache uwanjani kufunga mabao kumzidi Sarpong ambaye naye ametua Yanga msimu huu.
Katika Ligi Kuu Bara, Mugalu raia wa DR Congo, amefunga mabao manne akiwa amecheza mechi saba, huku Mghana, Sarpong akifunga mabao hayo kwenye mechi 15 za ligi.
Jumla Mugalu ametumia dakika 249 kwenye mechi saba kati ya mechi 15 ambazo Simba imecheza na ikiwa imefunga jumla ya mabao 37 yeye alifunga mabao manne akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 62.
Sarpong ametumia jumla ya dakika 1,085 na amecheza mechi 15 ndani ya Ligi Kuu Bara kati ya 18 ambazo timu hiyo imecheza msimu wa 2020/21 ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 271.
Mechi 8 aliyeyusha dakika zote 90 ndani ya uwanja akimpoteza Mugalu ambaye ni mechi moja kati ya saba ambazo ameyeyusha dakika zote hizo.Muda wa Mugalu ni: Biashara United (dk 14), Gwambina (dk 16), JKT Tanzania (dk 90), Kagera Sugar (dk 27), Mbeya City (dk 45), KMC (dk 33), Ihefu (dk 24).
Kwa upande wa Sarpong ni: Tanzania Prisons (dk 90), Mbeya City (dk 90), Kagera Sugar (dk 90), Mtibwa Sugar (dk 88), Polisi Tanzania (dk 27), KMC (dk 90), Biashara United (dk 90), Gwambina (dk 32), Simba (dk 68), Namungo (dk 90), Azam FC (dk 20), Ruvu Shooting (dk 85), Mwadui (dk 90), Dodoma Jiji (dk 45) na Prisons (dk 90).
Kinara wa utupiaji wa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara ni nahodha wa Simba,mshambuliaji bora wa muda wote ndani ya ardhi ya Bongo, John Bocco mwenye mabao nane na pasi mbili za mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment