January 22, 2021

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa nyota wao mpya Bernard Morrison hasumbuliwi na tatizo lolote bado yupo imara licha ya habari kueleza kuwa anaumwa.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa Morrison ambaye ni ingizo jipya ndani ya Simba akitokea Klabu ya Yanga anaumwa na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita akifanyiwa matibabu.

Kwenye Kombe la Mapinduzi hakucheza mchezo hata mmoja kati ya minne na alionekana benchi kwenye mchezo dhidi ya mabosi wake wa zamani Yanga ambao ulikuwa ni wa fainali ila hakucheza aliishia benchi.

Kaimu Kocha, Seleman Matola amesema kuwa hakucheza mchezo huo kwa kuwa hakuwa fiti kiafya.

Leo Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mchezaji huyo ni mzima na hana tatizo.

"Morrison ni mchezaji hana tatizo yupo fiti na ataonekana uwanjani hivi karibuni hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu mchezaji wetu," .

4 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Wananchi Wana Nini si tunawaona matahira tu,au mazumbukuku ulimwengu uko huku kazi yenu kuongopewa Kila siku

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic