January 22, 2021

 


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Waziri Junior amesema kuwa anaamini kuwa upo uwezekano wa kikosi chao kuibuka na ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu bila kupoteza mchezo hata mmoja. 

Waziri aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea kwenye kikosi cha klabu ya Mbao aliyoichezea msimu uliyopita tayari ameifungia Yanga bao moja akilifunga kwenye mchezo wa raundi ya kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-1 walioupata dhidi ya KMC.

Licha ya kuwa na mwendo wa kusuasua ndani ya Yanga lakini nyota huyo akiwa na Mbao msimu iliyopita alimaliza akiwa kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa wafungaji bora baada ya kuweka kambani mabao 13.

Akizungumzia ubora wao msimu huu Waziri amesema: “Tumekuwa na msimu mzuri tangu kuanza kwa ligi na ndiyo maana mpaka sasa kikosi chetu kinaongoza msimamo wa ligi na hatujapoteza mchezo wowote.

“Ubingwa tulioupata kupitia michuano ya kombe la Mapinduzi umezidi kutupa ari ya kupambana zaidi na naamini tutafanya vizuri kwenye michezo ya mzunguko wa pili ambapo tunataka kutwaa ubingwa, na kama tutaendelea kupambana namna tunavyopambana basi inawezekana tukatwaa ubingwa bila kufungwa,”

4 COMMENTS:

  1. MTAMBO WA MABAO, HAYA ONGEZA JUHUDI

    ReplyDelete
  2. Wewe mgosi weweee!! Mechi zenyewe hupangwa utaikeiya du benchi haafu waabwabwaja! Eka washu wene mbwanga

    ReplyDelete
  3. Ubingwa bila kufungwa aliweza Mnyama, wewe UTOPOLO huwezi utapigwa tu na ubingwa wenyewe hutapata

    ReplyDelete
  4. Yaani waziri junior nae ni mtambo wa mabao?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic