ANAYESEMEKANAkuwa baba wa nyota wa Klabu ya Simba, Meddie Kagere, Vedasto Katologi ameibuka na kusema yeye ni baba wa nyota huyo.
Katologi ameliambia Championi Jumamosikuwa, alimpata Kagere baada ya kuwa na uhusiano na mwanamke wa Burundi ambaye hamkumbuki lakini anafahamu kuwa ndiye aliyemzaa staa huyo wa Simba.
Aliongeza kuwa hakumbuki jina la mwanamke huyo ambaye ni mama wa Kagere ila alianza kuhisi kuwa nyota huyo ni mwanaye baada ya kujiunga na Klabu ya Simba.
Championi Jumamosiambalo lilizungumza live na Katalogi kwenye makazi yake Mbezi Makabe jijini Dar, alifunguka vitu kibao kuhusiana na ishu hiyo ambavyo vingine utavipata live kupitia Global TV Online.
“Baada ya Meddie kujiunga na Simba nilipata taarifa kutoka kwa watu mbalimbali wa soka kipindi hicho mimi nilikuwa sifuatilii sana michezo ila nilianza kuangalia kwa ajili ya mwanangu (Kagere).“
Nilimtafuta Kagere akaniambia atanitafuta na kunitumia hela ya nauli ili nije Dar tuonane ila amekuwa kimya hata nikimtafuta hajibu.“
Nilifanya juhudi za kutafuta nauli na kuja Dar ili kuonana naye ila zikashindikana nikaishia kumuona meneja wa Simba akaniambia kuwa Kagere amesema hana ndugu hapa Tanzania ndugu zake wote wapo Afrika ya Kusini.“
Ninachoomba Waandishi wa Habari wewe nisaidie mimi kuonana naye nataka kupima naye DNA, kama hatakuwa mwanangu ni sawa na nitakuwa nimeridhika kuliko kukaa na maswali mengi kichwani, mimi sina shida na mali zake nataka kijua ukweli tu.
Huyu nae asitutoe kwenye reli tuna mechi kubwa keshokutwa. Muda wote huu alikuwa wapi hadi kagere ana zaidi ya miaka 30? Ni wale wale wanaotumika kuvuruga hali. Kufanana sio lazima uwe ndugu
ReplyDeleteKama mwanamke humkumbuki hata jina unajuaje Kama ndiye aliyemzaa staa huyo.... Atakuwa anatumika huyu ili kuvuruga
DeleteSura haipotezi huyo ni kagere bopy to right wala haihitaji DNA
ReplyDeleteSura haipotezi huyo ni kagere bopy to right wala haihitaji DNA
ReplyDeleteSura haipotezi huyo ni kagere bopy to right wala haihitaji DNA
ReplyDeleteHana kitu huyu hata kama ana hoja why kipindi hiki? Mimi nahisi ni wale wale
ReplyDeleteUtadhani bongo movie
ReplyDeleteHuyo anatafuta umaarufu tu Na kuvuruga mambo
ReplyDeleteSiku zote alikuwa wapi, kagere msimu watatu huu yupo Simba hakujitokeza, kukamata Tia makofi upumbavu wakuvurugana peule hatuutaki
ReplyDeleteWaandishi mnatumika vibaya kwann msiache mechi ipite kwanza ndo mlete hayo maujinga yenu
ReplyDeleteSiku zote waandishi wa mpira wako kwa maslahi yao binafs hilo siwez laum moja kwa moja lakn kna wakat busara itumike yawezakana n baba take Kagere lkn kna haja gam kuweka mambo mwenye media.Huu n upuuz kabisa na haifai kusoma madudu kama haya
ReplyDeleteMwandishi maandazi, sasa unapiandika baba wa kagere ina maana una hakika na hilo? Ulipaswa kuandika anayedai kuwa baba wa kagere na sio kujiamulia tuu. Anayejua baba halisi wa kagere ni mama wa kagere na sio wewe mtumwa wa upande ule.
ReplyDelete