KOCHA mkuu wa klabu ya
Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake
kitatwaa ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi katika fainali dhidi ya
Simba itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja.
Yanga imetinga hatua ya
fainali ya michuano hiyo baada ya kuiondosha klabu ya Azam kwa changamoto ya
mikwaju ya penalti 5-4 kwenye hatua ya nusu fainali iliyopigwa jana Jumatatu.
Akizungumzia mchezo huo wa
fainali Kaze amesema: “Tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapata matokeo
chanya kwenye mchezo wetu wa fainali dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumatano.
“Tunajua utakuwa mchezo mgumu na wenye presha kubwa, lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ubingwa wa michuano hii, ili kuzidisha morali ya kufanya vizuri zaidi pale tutakaporejea kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara," .
Hii inakuwa ni fainali ya kwanza kwa Kaze kuingoza Yanga kupambana na Simba kwenye Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Kaze kwenye mechi tatu ambazo ameongoza vijana wake ni mechi moja waliruhusu bao ilikuwa kwenye sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC huku vijana wake wakiwa wamefunga mabao mawili.
Mchezaji wa kwanza kufunga alikuwa ni Zawadi Mauya alifunga mbele ya Namungo FC na wa pili alikuwa ni Tuisila Kisinda.
Habari hii hii inapostiwa mara mbili kwa kubadili picha tuu?
ReplyDeleteHata Mimi nimeliona huyu mwandishi ni kiboko wa kusaka wasomaji
ReplyDelete