AYOUB Lyanga nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amefunga bao liliweka usawa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo, uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Lyanga alifunga bao hilo dakika ya 57 kipindi cha pili baada ya DR Congo kutangulia kufunga bao la kwanza kipindi cha kwanza.
Congo ilipachika bao dakika ya 19 kupitia kwa Fiston Mayela ambaye alipiga shuti kali akiwa nje ya 18 na mlinda mlango Juma Kaseja alikwama kuokoa baada ya kuteleza kabla ya kuokoa mpira uliozama wavuni.
Pongezi kwa Ditram Nchimbi aliyetoa pasi ya bao iliykutana na Lyanga ambaye aliwanyanyua mashaki dakika ya 57 Uwanja wa Mkapa.
Pia mkongwe Agrey Morris aliweza kutumia dakika 2 kwenye mchezo wa leo ikiwa ni mara yake ya mwisho kutumika ndani ya Stars baada ya kuomba kustaafu.
Kocha Mkuu wa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa wachezaji wake wengi ni wapya jambo linalomfanya ajenge muunganiko mzuri wakati ujao.
Tunaenda kwenye mashindano ya CHAN na wachezaji wapi, huo muda wa kupata muunganiko unatoka wapi?
ReplyDeleteHata uteuzi wetu wa makocha wa timu ya taifa stars ni Tia maji Tia maji. Watanzania tutavuna tunachokipanda. Tumeamua kuajiri kocha wa kawaida tutapata matokeo ya kawaida.Makocha wa mwendo Kasi wamejaa tele.Hata muheshimwa rahisi huajiri wasaidizi wa mwendo Kasi ili apate matokeo yenye ubora na Kasi kiutendaji. Tatizo la watanzania hatujui thamani yetu.Hatuna hamu ya kuwaza mafanikio makubwa na kuanza kuyafanyia kazi kivitendo.Gorani coupuvinic aliekuwa kocha wa Simba aliewaibua akina ndemla Kama serikali na TFF wangeuma meno na kumuajiri kwa muda mrefu basi leo watanzania tungekuwa taifa lenye kuheshimika kisoka. Inawezekana ghorani angekuwa ghali kidogo kumlipa ila Kama Simba iliweza kumuajiri kwanini Kama nchi nzima tushindwe? Ghorani ni kocha anaeunda utambulisho wa Aina ya mpira wa timu fulani. Kwa sasa Taifa stars hatujui tunacheza mpira wa aina gani? Ila miraji athumani,muzamiru yasini na Dilunga hata shabalala tukiachana na upenzi Kama ningekuwa kocha wa Taifa stars na benchi lake ningewachukuwa sio kama wazuri sana bali wangemrahisishia kazi mwalimu kuingunusha timu kwa kipindi kifupi kabla ya mashindano na maoni sio maombi ni fikra za mtu binafsi povu ruksa.
DeleteWachezaji wapya
ReplyDeleteKocha aache swaga...kama timu imemshinda abwage manyanga
ReplyDeleteTATIZO LA USIMBA NA UYANGA LIMEIANDAMA NCHI....LEO ILIKUWA TAIFA STARS LAKINI WAANDISHI WANAONGELEA MAMBO YA SIMBA SIMBA KWANINI HII KANSA HAIONDOLEWI KWENYE UBONGO WA WATANZANIA???? UNAULIZA MASWALI KWA KOCHA KUHUSU SIMBA WAKATI WALIOCHEZA LEO NI TAIFA STARS NA DRC CONGO???
ReplyDelete