January 7, 2021


 ADAM Adam, nyota wa Klabu ya JKT Tanzania ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na michuano ya CHAN amesema kuwa atasaini Simba ikiwa watampa dili lenye maslahi mazuri.

Adam mwenye mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara na pasi moja ya bao amekuwa akitajwa kuhitajika ndani ya Klabu ya Yanga ambayo ilianza kumpigia hesabu pamoja na Simba zote zenye makazi yao pale Kariakoo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Adam mwenye rasta kichwani amesema kuwa amepata ofa nyingi ndani ya ardhi ya Bongo pamoja na nje jambo analosubiri ni kuona wapi kutakuwa na ofa kubwa.

“Kwa Bongo timu kubwa zimekuwa zikinifuata na zinahihitaji kupata saini yangu. Kwangu mimi sina tatizo hata Simba ninasaini ikiwa tu wataweka ofa nzuri ambayo itakuwa na maslahi kwangu.

“Kikubwa kwa mchezaji ni kuona anapata nafasi ya kupata changamoto mpya na ninaamini katika uwezo wangu ninaweza kufanya vizuri zaidi hivyo ni suala la muda tu.


"Kuwa ndani ya Stars pia kunanifanya nizidi kuongeza juhudi ili niwe bora kwani hakuna ambaye anapenda kuitumikia timu yake ya taifa hilo lipo wazi kwa kila mchezaji," amesema.


Januari 10, Stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo, Uwanja wa Mkapa.

6 COMMENTS:

  1. NENDA KAUE KIPAJI NENDA KASTAAFU SOKA KIJANA, KESHO UKIPELEKWA KWA MKOPO IHEFU USIGOME KIJANA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asikuumize kichwa huyu mwandishi maana ndo zake kuwapigia promo wateja wake

      Delete
  2. Simba haimuhitaji ila ndio sehemu sahihi kabisa ya kukuza kipaji chake na kuwa wa kimataifa kama anaweza ushindani. Kwa hapa Adam ndie mwenye kuihitaji simba zaidi kama kweli anataka kutoka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ana kzi kubwa ya kufanya hapa, asipoangalia yatamkuta ya SALAMBA, AU WAKINA MIRAJI NA AJIBU

      Delete
  3. Salamba, Kaheza, Miraji Athumani, Rashidi Juma, Gadiel, Hajib, na wengine wengi wanajuta kuzaliwa....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic