February 21, 2021

 



BAADA ya kuipa Yanga pointi tatu muhimu katika mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar, kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Angola, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ amesema kuwa amejipanga vizuri kuisaidia timu yake baada ya kurejea kutoka kwenye majeruhi.

Carlinhos alifunga bao hilo dakika ya 73 ya mchezo akimalizia pasi ya Mkongomani Tuisila Kisinda, dakika moja tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Ditram Nchimbi.

Bao hilo linamfanya Carlinhos aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu mpaka sasa awe amehusika kwenye mabao matano ya Yanga msimu huu akifunga mabao matatu na kuasisti mara mbili.

Akizungumzia uwezo wake kwenye mchezo huo Carlinhos amesema: “Nimefurahi kuona narejea kwa kasi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa na majeraha.

“Ushindi huu umezidi kunipa nguvu ya kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo na naamini nitafunga na kujitahidi kutengeneza mabao mengi zaidi kwa ajili ya mafanikio ya kikosi changu,"

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic