UONGOZI wa Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola ambao ni wapinzani wa Namungo katika michezo ya mtoano ya kombe la Shirikisho Afrika, umelalamika kufanyiwa hujuma na Watanzania baada ya wachezaji wao watano wa kikosi cha kwanza kutajwa kuwa na maambukizi ya COVID-19.
Kupitia mitandao yao ya kijamii 1de Agosto walitoa
taarifa iliyoeleza kama ifuatavyo: “Dakika ya mwisho wachezaji wetu watano
wamedhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona kupitia vipimo vilivyoonyesha
wana maambukizi.
“Hili limefanyika ili kudhoofisha timu yetu, Watanzania kwa makusudi
na dhahiri kabisa wanadai kuwa wachezaji wafuatao wana maambukizi ya COVID-19:
Kipa Neblú, mabeki wa kati Bobó na Boni, kiungo Mário na mshambuliaji Mabululu,
pamoja na Mratibu wa timu ya Untonesa Sampaio.
“Habari hii ilifika saa saba mchana kwa saa za Tanzania, na italazimisha benchi letu la ufundi kufanya mabadiliko ya kikosi cha wachezaji 11 waliotarajiwa kuanza,”
Ikumbukwe kuwa wakiwa nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa
kwanza uliopangwa kufanyika Februari 14, mwaka huu nyota watatu wa Namungo na
kiongozi mmoja walitajwa kuwa na maambukizi ya Corona na kusababisha
sintofahamu iliyopelekea mchezo huo kufutwa.
Baadae kamati maalum ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), ilifikia
maamuzi ya kuamuru michezo yote miwili kupigwa hapa Tanzania.
Hujuma ya nini tena?
ReplyDeleteMuda walioekwa ndani vijana wetu kule Angola basi sisi tuzidishe mara mbili zaidi kuwaweka ndani baadhi ya wachezaji wao hapa Tanzania waliokutwa na korona maana mpaka vijana wetu wapo Angola.
DeleteMwosha huoshwa
ReplyDeleteNilitaka kusema hivyo hivyo, walijisahau kuwa ulikua hili wenzako wanajua lile
ReplyDeleteUkijua hili wenzako wanajua lile
ReplyDeleteAnaejua Anajua tu,hujuma haiwezi kusaidia, tuache mchezo utawale...
ReplyDeleteUngeyasema hayo pindi Namungo walipokuwa Angola wakafanyiwa figisufigisu tungekuelewa vinginevyo tunaona thamani ya kichwa ni kwenye kufugia nywele tu
DeleteSafi sana.Nimependa jinsi uongozi wa Namungo ulivyopokea maoni yetu na kuyafanyia kazi.
ReplyDeleteNilisema kama wao wamemwaga mboga basi nasi tuumwagie ugali oil chafu.
Hao wachezaji wapelekwe lockdown JKT Ruvu kwa siku 14
Saaafi sana wamezoea kuwaonea watz
ReplyDelete