IKIWA tetesi zinaeleza kuwa Ettiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzana, Taifa Stars amesitisha mkataba wake, Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) limesema kuwa lina utaratibu maalumu wa kutoa taarifa.
Ndayiragije alishindwa kukiongoza kikosi cha Stars nchini Cameroon kutinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Chan ambayo yanawahusu wachezaji wa ndani nchini Cameroon.
Kutokana na kuboronga huko inaelezwa kuwa amechimbishwa ndani ya Stars ili kuweza kumpata kocha mpya ambaye atakuwa ndani ya Stars.
Stars ilikusanya pointi nne baada ya kucheza mechi tatu, ilishinda moja, sare moja na ilichapwa mechi moja ya ufunguzi kwa mabao 2-0.
Kombe la Chan limekwenda tena nchini Morocco ambao walikuwa ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambalo walilitwaa 2018 na kulifanya taifa hilo kutwaa taji hilo mara mbili.
Mleteni Sven aliekuwa kocha wa simba atatusaidia sana. Keshafundisha Cameroon Zambia na tayari anawajua wachezaji wetu.
ReplyDeleteMnatafuta makocha wa nje?wakati tunao wakina moroko
ReplyDeleteMorocco alishapewa taifa stars akafeli.
ReplyDeleteTatizo la stars sio kocha hata akiletwa clop tutafungwa tu.
ReplyDeleteSuluhisho hapa ni kuwa na soka la vijana ambao tukiwatunza vizuri watatuletea mafanikio sana na si kocha
ReplyDeleteSuluhisho hapa ni kuwa na soka la vijana ambao tukiwatunza vizuri watatuletea mafanikio sana na si kocha
ReplyDeleteNasikiaba wanataka wamlete Pep Guadiola kutoka Man City, sijui kweli?! Au nimesikia vibaya?!
ReplyDelete