February 10, 2021

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kinatarajiwa kuanza safari ya kuwafuata wapinzani wao Mbeya City, jiji Mbeya, kesho Februari 11.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi zao 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 wana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, Februari 13. 

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa baada ya ule mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Mbeya City kuacha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Lamine Moro kwa kichwa akitumia kona ya Carlos Carinhos,mwenye pasi mbili na mabao mawili ndani ya Yanga.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema timu itaondoka jijini Dar es salaam ikiwa na wachezaji 24 na viongozi 18, nane wakiwa wa benchi la ufundi

"Timu itaondoka Dar Alhamisi, tutaondoka na wachezaji 24 na viongozi 14, tutakuwa na msafara wa watu 38.

"Jumamosi tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Mbeya City lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda, lengo letu ni kutwaa ubingwa msimu huu," amesema.

Kaze kuhusu mchezo huo amesema kuwa anatambua utakuwa na ushindani mkubwa ila wanahitaji kupata pointi tatu.

"Tunawaheshimu Mbeya City ni timu imara nasi tutaingia ndani ya uwanja kwa mpango mzuri wa kusaka pointi tatu hivyo mashabiki watupe sapoti,".

Miongoni mwa wachezaji ambao watabaki Bongo ni pamoja na Dickson Job na Saido Ntibanzokiza ambao wapo na program maalumu pamoja na kipa namba tatu, Ramadhan Kabwili.

3 COMMENTS:

  1. Utakuwa mwepesi sana ukilinganisha na Yanga kwasababu Mbeya City ni kati ya timu zilizopo mkiani

    ReplyDelete
  2. Mbeya City ni yapili kutoka chini na ipo hatihati kuteremka daraja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic