February 21, 2021

 K


KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amekiri kuwa ni kweli ndani ya kipindi cha wiki moja iliyopita alikuwa katika mazingira magumu kutokana na presha ya matokeo mabaya ambayo kikosi chake kilikuwa kikipitia.

Kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka huu, Yanga juzi Jumamosi iliibuka na ushindi  kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam, hii ni baada ya kupata matokeo ya sare tatu mfululizo.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 49 baada ya kucheza michezo yao 21 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi.

Akizungumzia presha aliyokuwa akikumbana nayo Kaze amesema: “Tunashukuru kwa kupata ushindi kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.

"Ni kweli ndani ya wiki moja iliyopita nimepata kujifunza vitu vingi kuhusu utamaduni wa soka la Tanzania, timu yetu haikuwa na matokeo mazuri na presha ilikuwa kubwa kwangu.

"Wachambuzi walikuwa wakitukosoa sana kiasi cha mashabiki wetu kupoteza imani, siwezi kubadilisha utamaduni huo lakini nikiri kuwa wiki moja iliyopita ilikuwa ngumu sana kwangu, lakini nimepata kujifunza mambo mengi pengine hata kuliko muda wote niliokuwepo Tanzania,"


3 COMMENTS:

  1. BADO HAUJAJIFUNZA MUANGALIE MWINYI ZAHERA KWANZA, UTAPATA MAJIBU

    ReplyDelete
  2. 1. Ubishi utakuponza: Kuondoka kwa Mwambusi utakujutia pamoja na kuchelewa kufanya sub, hata inapoonekana wazi mbinu mlizopanga zimegonga mwamba
    2. Uzoefu wa ligi yetu katika hatua hii na mazingira yaliyopo hivi sasa (kufukuzana na Simba) yanahitaji nguvu, mbinu na ubunifu zaidi kutoka kwenye Benchi lako la ufundi na viongozi
    3. Mlengo wako wa kuwabeba baadhi ya mastaa utakutokea puani. Kuna baadhi ya machaguo yako hayana tija kabisa. Mchezaji wa kimataifa anakuwa na pass accuracy chini ya 40%?
    5. Mipira ya kutengwa: Timu inapoteza kona zote na mipira yote ya adhabu ndogo! Upigaji ni mbovu na hata hakuna mawasiliano na wanaopigiwa!
    Mabeki wa kati ws Yanga, pamoja na urefu wao, hawaruki kuokoa krosi au kona zinazopigwa kwao!
    Jipange sivyo utasepa kabla ya Mei, 20

    ReplyDelete
  3. Sio muda mrefu watakufukuza...yanga sio watu wazuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic