February 21, 2021

 

 


KOCHA mkuu wa kikosi cha Mtibwa Sugar, Hitimana Thierry amesema kuwa, miongoni mwa vitu vilivyowaponza mpaka kupoteza mchezo wao wa jana dhidi ya Yanga ni maamuzi ya kumuuza kitasa wake Dickson Job.

Job alijiunga na Yanga akitokea   Mtibwa  katika kipindi cha dirisha dogo la Januari lilikofungwa     Januari 15.

Mtibwa juzi Jumamosi ilipoteza mbele ya Yanga kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kipigo hicho kimeifanya Mtibwa Sugar kusaliwa na pointi zao 23 zinazowaweka katika nafasi ya 11 ya msimamo, baada ya kucheza michezo 20 huku wakiwa hawajapata matokeo ya ushindi tangu Desemba 19, mwaka jana.

Akizungumzia mchezo huo Thierry amesema walifanya kosa kubwa kumruhusu Job kuondoka kwani pengo lake mpaka sasa bado halijazibwa.

“Kile ambacho tulikihofia ndicho ambacho kimetokea kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Yanga, tangu kuondoka kwa beki wetu Dickson Job ambaye alijiunga na Yanga Januari mwaka huu hatukupata mbadala wake.

“Hiyo imepelekea kuwepo makosa mengi katika safu yangu ya ulinzi ambayo yanapelekea tunaadhibiwa, kama ambavyo imetokea kwenye mchezo dhidi ya Yanga.


 

5 COMMENTS:

  1. Sisi inatuhusu nn huo Ni upumbavu wenu

    ReplyDelete
  2. Kilichowaponza ni uwepo wa Kessy kwenye kikosi cha mtivea. Inajulikana yule ni agent wa yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha hizo wewe dogo, mbona maagent wa Simba walikuwepo kibao, wasizuie bao?

      Delete
    2. Kessy aliacha nafasi wazi kwa makusudi ni yuda katika timu ya mtibwa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic