MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa licha ya kwamba wachezaji wake uwanjani walibaki 9 walijitahidi kufanya kazi kubwa ndani ya Uwanja wa Molineux.
Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 2-1 ikiwa ugenini mbele ya Wolves ambapo wachezaji wake wawili ambao ni David Luis dakika ya 45 na Bernd Leno dakika ya 72 walionyeshwa kadi nyekundu.
Mabao ya Wolves ambayo ipo nafasi ya 14 na pointi zake 26 baada ya kucheza mechi 22 yalifungwa na Ruben Neves dakika ya 45+3 kwa penalti na Joao Moutinho alipachika bao la pili dakika ya 49.
Kwa Arsenal, Nicolas Pepe alifunga bao la kwanza ambalo halikulindwa na Arsenal dakika ya 32 na kuwafanya wabaki na pointi zao 31 wakiwa nafasi ya 10 na imecheza mechi 22 ndani ya Ligi Kuu England.
"Wachezaji walijitahidi kipindi cha pili kuonyesha juhudi licha ya kuwa walikuwa tisa uwanjani. Kipindi cha kwanza ilikuwa ngumu kuweza kupata ushindi ila kipindi cha pili mambo kidogo kulikuwa na mabdailiko.
"Ni matokeo mabovu kwetu ila bado ni mwanzo mzuri na ninaona kwamba wachezaji wanajitahidi kufanya vizuri ndani ya uwanja," .
0 COMMENTS:
Post a Comment