KASI ya washambuliaji Opah Clement wa Simba Queens na Aisha Masaka wa klabu ya Yanga Princess kwenye Ligi Kuu ya Wanawake, inaashiria wazi kuwa nyota hao wamejipanga kuumaliza ufalme wa mshambuliaji wa JKT Queens Fatuma Mustapha katika vita ya ufungaji bora msimu huu.
Mabao saba aliyoyafunga Opah kwenye mchezo wa mwisho wa
mzunguko wa kwanza dhidi ya TSC Queens yamemfanya afikishe mabao 20 na kumfikia
Fatuma aliyekuwa akiongoza chati ya wafungaji, huku Masaka yeye akiwa tayari
ameweka kambani mabao 15.
Akizungumzia malengo yake Masaka amesema : “Kwanza najisikia furaha kuwa sehemu ya kikosi
cha klabu ya Yanga na kwa kuanza vizuri msimu huu kwa kufunga mabao 15 mpaka
sasa, malengo yangu ni kupambana kuisaidia Yanga kuibuka na ubingwa msimu huu,
lakini kama mshambuliaji nataka pia kuibuka na tuzo ya ufungaji bora,”
Haya jitahidi
ReplyDelete