February 3, 2021

 

 


BONDIA wa ngumi za kulipwa, Mfaume Mfaume amefunguka kuwa siri kubwa ya ushindi wa Bondia Ibrahim Class kwenye pambano lake la usiku wa Ijumaa iliyopita dhidi ya Mmalawi Danis Mwale ni uwezo wake mkubwa wa kutumia kwa ufasaha ngumi yake ya kulia kupata pointi.

Katika pambano hilo la raundi 12 lililopigwa kwenye ukumbi wa Next Door, Class aliibuka na ushindi wa pointi na kutwaa mkanda wa WBF intercontinental uzito wa Super Light.

Akizungumzia ubora alionao Class Mfaume amesema: “Tangu nimeanza kumfahamu Ibrahim Class najua ni mtu ambaye anatumia akili nyingi sana kwenye mapambano yake,.

"Silaha yake kubwa ni ngumi yake kali ya mkono wa kulia ‘right’ yake ambayo huitumia kuongeza pointi kwani mara nyingi huwa inafika inapokusudiwa.

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic