February 3, 2021

 



USAJILI wa washambuliaji Matheo Anthony kutoka KMKM na Charles Ilanfya kutoka Simba katika kipindi cha dirisha dogo umewapa kiburi ‘Wanakinoboys’ KMC ambao wametamba kufanya vizuri katika michezo yao ya mzunguko wa pili.

Ilanfya amejiunga na KMC aliyoichezea msimu uliopita kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita, kufuatia kuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya kikosi cha klabu ya Simba ambapo alifanikiwa kukichezea kikosi hicho mchezo mmoja pekee.

Ilanfya tayari ameanza mazoezi na kikosi cha KMC kinachojiandaa na mchezo wa kiporo cha ligi dhidi ya Namungo utakaopigwa kesho Alhamisi.

Akizungumzia maboresho ya kikosi chao kupitia usajili,  Ofisa habari wa klabu ya KMC, Christina Mwagala amesema usajili huo wa maboresho umewafanya kuwa na kikosi imara zaidi ambacho kitawasaidia kufanya bora zaidi. 

“Kikosi chetu kinaendelea na mazoezi makali ya kujiandaa na michezo yetu ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara chini ya kocha mkuu John Simkoko na msaidizi wake Habibu Kondo, na kwa kuanzia tutamalizia mchezo wetu wa kiporo dhidi ya Namungo siku ya Alhamisi.

“Tunaamini mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Namungo lakini tumejipanga kuibuka na pointi tatu muhimu,” 

Akiwa na kikosi cha KMC msimu uliopita Ilanfya alifanikiwa kuweka kambani mabao 6


1 COMMENTS:

  1. Utarejea nyumbani na nguvu mpya na huko umepelekwa ukanolewe na Utarejea uso juu kumchukuwa nafasi yako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic