HABARI njema kwa kikosi cha klabu ya Azam ni kurejea kwa nyota wao wawili waliokuwa na majeraha, Salumu Abubakar ‘Sure Boy’ na Aggrey Morris.
Sure Boy na Morris walipata majeraha hayo katika mazoezi ya
kikosi chao kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, mchezo
iliopigwa siku ya Jumamosi.
Azam jana ilicheza dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa
kimataifa wa Kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini
Dar es Salaam na kushuhudua Azam ikilazimishwa sare ya bao 1-1.
Akizungumzia hali za nyota hao Mkuu wa kitengo cha habari na
mawasiliano wa klabu ya Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema nyota hao tayari wamefanya
mazoezi ya pamoja na wenzao.
“Ni kweli wachezaji wetu wawili, Sure Boy pamoja na nahodha,
Aggrey Morris walipata majeraha katika maandalizi yetu kuelekea mchezo wa
Jumamosi iliyopita dhidi ya KMC.
“Lakini hayakuwa majeraha makubwa kwani tayari wamerejea
uwanjani na kufanya mazoezi ya pamoja na timu,”
0 COMMENTS:
Post a Comment