BAADA ya kuanza rasmi mazoezi na kikosi cha klabu ya Yanga, mshambuliaji hatari wa timu ya Taifa ya Burundi, Fiston Abdoul Razak ameahidi kujituma kuifungia klabu hiyo mabao mengi ili kuisaidia katika vita ya kusaka ubingwa msimu huu.
Fiston aliyetua rasmi siku ya Ijumaa akitokea nchini Burundi, na kupelekwa moja kwa moja kujiunga na kambi ya timu hiyo anakamilisha idadi ya wachezaji watatu waliosajiliwa na Yanga katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo.
Wachezaji wengine wa Yanga waliosajiliwa ni; Dickson Job na
Saidi Ntibazonkiza, huku Yanga pia ikiongeza nguvu kwenye benchi lake la ufundi
kwa kumwajiri kocha msaidizi Nizar Khalfan na kocha wa viungo raia wa Ghana
Edem Mortotsi.
Akizungumzia mipango yake Fiston amesema: “Nimejiandaa kuhakikisha najituma kwa uwezo wangu wote, ili kufunga mabao mengi na kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa msimu huu,”
Atafunga sana mazoezini
ReplyDeleteAkiba ya maneno ingefaa
Delete