ZIKIWA zimebaki siku tatu pekee kabla ya kuwavaa Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, presha imeshuka ndani ya kikosi cha Yanga baada ya wachezaji watatu kati ya wanne waliokuwa majeruhi kuanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzao.
Nyota walioanza mazoezi na wenzao wanaojiandaa na mchezo wa Mbeya City ni beki Dickson Job na washambuliaji, Yacouba Sogne na Michael Sarpong huku kiungo mshambuliaji Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ akiwekwa chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu hiyo.
Saido ambaye amehusika kwenye mabao matano ya Yanga akifunga mabao mawili na kuasisti mara tatu, bado anasumbuliwa na matatizo ya misuli ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.
Akizungumzia hali ya nyota hao, Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema kikosi hiko kinaendelea na maandalizi ya mwisho tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City.
“Kikosi chetu kinaendeleda na maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Mbeya City, tunashukuru kuwa kati ya wachezaji wanne waliokuwa na majeraha watatu tayari wameanza mazoezi ya pamoja na wenzake.
“Sarpong, Yacouba na Job wote wako vizuri aliyebaki ni Saido ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari wanaoangalia maendeleo yake,” alisema Saleh.
Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa
ligi na pointi zao 44 walizokusanya katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa
wakishinda mechi 13 na kutoa sare kwenye michezo mitano.
Ulinzi wa nini bila ya shaka wansogopa asije kutafunwa na kumezwa mzimamzima na Simba
ReplyDeleteSimba anayemtegemea paka mweusi?
DeleteSio bure lazima utakuwa Mwanga tu wewe, Kama unaamini Paka anaweza kuleta ushindi kwenye Mpira lazima utakuwa kigagula
DeleteSi mlimpeleka wenyewe... kuna timu nyingine iliyofanya hivyo? akili za kimanga kunuka koko
Delete